Search This Blog

Friday, August 20, 2021

CCM yaitaka serikali kulipa malipo ya kazi alizokwishafanya mkandarasi wa barabara ya kutoka kazilambwa hadi Chagu


KAMATI ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora imeomba kumlipa kiasi bilioni 2 Mkandarasi STECOL Corporation ambazo anadai kufuatia kazi alizokwishafanya katika mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Kazilambwa mkoani Tabora hadi Chagu mkoani Kigoma.

Kauli hiyo imetolewa leo Wilayani Kaliua na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi wakati wa ziara ya Kamati kukagua miradi ya maendeleo,

Alisema Serikali inapaswa kumlipa kutokana na hati tatu ambazo ameshawasilisha ili kumwezesha kuendelea kwa kasi kwa kazi zilizobaki.

Aidha Mwenyekiti huyo alimtaka Mkandarasi kuhakikisha anajenga mapema na kiwango cha juu eneo korofi la Kazilambwa ambalo wakati wa masika linakuwa na maji mengi na wakati mwingine kusababisha kutopitika.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania(TANROADS) Mkoa wa Tabora Damian Ndabalinze(kushoto) alisema kuwa kazi ya ujenzi wa barabara hiyo umefikia asilimia 15 na unaurefu kilometa 36 na utagharimu bilioni 32,4 hadi kukamilika.

Alisema mradi huo umekuwa ukipenda polepole kutokana na uchelewashaji wa malipo kwa Mkandarasi hata baada ya kuwasilisha hati tatu(certificates)

Ndabalinze aliongeza kuwa mradi huo ulikuwa ukamilike Mwezi Novemba mwaka huu lakini hautakamika na hivyo wameomba Mkandarasi kuongezewa Miezi mitano.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amesema atawasiliana na Wizara ya ujenzi kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi ili kazi iendelee kwa kasi.

 




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...