Search This Blog

Sunday, July 4, 2021

Makamu wa Rais Dkt. Mpango arejea nchini akitokea Ufaransa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango hii leo Julai 4, 2021 amerejea  nchini  akitokea Paris nchini Ufaransa  alikoshiriki Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum)  akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es salaam, Makamu wa Rais amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makala pamoja na viongozi wengine wa ulinzi na usalama wa mkoa huo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...