Search This Blog

Monday, July 19, 2021

DC Kayanda awashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea taifa

 


Tunatambua mchango wa viongozi wa dini katika kujenga jamii ya watu waadilifu, na wenye maadili yaliyojengwa katika misingi ya kiimani. Kwa kupitia taasisi zenu za elimu tunapata wananchi wenye maarifa na weledi mbalimbali wa kitaaluma na kutujengea jamii ya wasomi. 

Mnasaidia wananchi katika kujenga afya za mwili kupitia huduma za kiafya katika taasisi za afya zinazosimamiwa na dini.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akifungua kikao cha viongozi wa dini katika ukumbi Karatu Lutherani. 


Amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kuliombea taifa kuwa na amani na kuendelea kuombea viongozi wa serikali katika majukumu yao ya uongozi. Amesema amani iliyopo ndio inawezesha wananchi kujikita katika shughuli za maendeleo.

Mh. Kayanda amesema serikali inathamini mchango wa viongozi wa dini, na kama kuna jambo viongozi wa dini wanataka ushirika na serikali wasisite kushauri. Serikali ipo tayari muda wowote kukutana na kuzungmza na viongozi wa dini. 


Mh. Kayanda amegusia swala la ugonjwa wa virusi vya corona na ameomba viongozi wa dini kuelimisha wananchi kupitia nyumba za ibada, waumini namna ya kuchukua tahadhari ili kujikinga na virusi hivyo. 

Amesema vyombo vya kunawia mikono kwa maji tirirka na sabuni vinaaswa kuwepo lakini pia vitakasa mikono na kuvaa barakoa ili kujikinga. Ameongeza kusema waumini katika nyumba za ibada wanapaswa kukaa kwa nafasi ili kuepuka kusongamana.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...