Search This Blog

Saturday, June 5, 2021

Simulizi ya bibi wa miaka 106 akataa kuitwa 'mzee'


Bi. Eileen Kramer mwenye umri wa miaka 106, anaonekana kuendelea na kazi zaidi licha ya umri aliokuwa nao.

Ameandika simulizi yake akiwa nyumba ya kuwaangalia wazee, anachapisha vitabu na ameingia katika mashindano makubwa ya uchoraji nchini Australia.

Baada ya miongo kadhaa ya kuishi nje ya nchi, Bi Kramer alirudi nyumbani Sydney akiwa na miaka 99. Tangu wakati huo, alishirikiana na wasanii kutengeneza video kadhaa kuonesha kipaji chake na mapenzi yake ya kucheza muziki.

Bi Kramer bado anacheza muziki - akiwa na neema, na kuonyesha miondoko ya kushangaza akiwa anatumia anatumia sehemu ya juu ya mwili wake.

Katika picha zake za miaka ya hivi karibuni, akiwa anacheza kwa kupendeza.

"Tangu niliporudi Sydney nimekuwa na kazi nyingi sana -Nilishiriki katika maonesho matatu makubwa ya muziki katika taasisi ya kitaifa ya sanaa ijulikanayo kama NIDA.

"Nilishiriki matamasha mawili makubwa huko Adelaide na Brisbane, Nimekuwa katika filamu , na nimefanya maonesho kadhaa madogo, nimeandika vitabu vitatu na leo nina muda wa kuzungumza na wewe!" amesema hayo akiwa nyumbani kwake.

Mara nyingine anaulizwa anapata wapi nguvu - na siri yake ni ipi inayomfanya aweze kucheza akiwa na umri mkubwa kiasi hicho.

Jibu lake huwa nimekataa neno "uzee" na "umri" katika misamiati yake. Na alinikata kumuita mzee katika mazungumzo yetu.

"Ninasema: Mimi sio mzee, Nimekuwa hapa muda mrefu tu na kujifunza mambo kadhaa.

"Huwa sihisi kile ambacho watu wanasema au wanataka tujihisi wakati tukiwa wazee.

Tabia yangu iko hivi tangu niko mtoto."

Miaka ya hivi karibuni Bi Kramer amekuwa mahiri katika umati wa watu kwa mitindo ya densi, amefanya kazi kadhaa za kucheza muziki katika maisha yake.

Alikuwa katika mpango wa kutengeneza video yake ya densi lakini hali ya kujifungia ndani iliyotokea Sidney ilivuruga mpango wake. Lakini si kwa muda mrefu. "Sikuweza kutoka nje kwenda kwenye eneo la kufanyia video, badala yake nliandika kitabu", alisema huku akicheka. "Hii ni hadithi kuhusu jinsi tulivyotengeneza filamu."

Eneo la kutengenezea filamu ni maalum kwa Bi Kramer. Lipo ndani ya Moreton Bay, mtini katika kitongoji cha Sydney cha Glebe.

Harufu ya miti, muonekano wa Moreton bay na sauti za ndege wakicheka huku wamekaa ni vitu vilivyo mshawishi Bi Kramer kurudi Sidney.

''Miti iliboresha mitino yangu ya kudensi'' alisema.

" Umewahi kuona...? unajisikia kama uko katika ikulu ya hadithi ya kusadikika. Inanikumbusha enzi za utoto"



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...