Rais wa Marekani (USA) Joe Biden aliidhinisha sheria ya "likizo ya serikali" ya Juni 19, ambayo inatambulika kama "Juneteenth" na kuadhimishwa kwa kumbukumbu ya utumwa katika nchi hiyo na kuwekwea marufuku mnamo mwaka 1865.
Biden, katika mkutano na waandishi wa habari aliofanya kwenye Ikulu ya White House, aliangazia historia ya utumwa nchini na kusema,
"Jamii kubwa hazipuuzi kumbukumbu zao zenye uchungu zaidi, bali huzikumbatia. Jamii kubwa hazitoroki makosa yao, bali hukubali na kukabiliana nayo."
Akizungumzia juu ya michango ya jamii ya asili ya Kiafrika nchini, Biden alisisitiza kuwa bado kuna kazi kubwa ya kufanywa kuhusu historia ya utumwa na tafakari zake.
Baada ya hotuba yake, Biden alisaini sheria ambayo hapo awali ilikuwa imepokea idhini kutoka kwa Baraza la Wawakilishi na Seneti ili kufanya Juni 19 kila mwaka kuwa likizo ya serikali.
Utumwa uliondolewa kikamilifu nchini Marekani mnamo Juni 19, mwaka 1865.

No comments:
Post a Comment