Search This Blog

Saturday, June 5, 2021

Mwanafunzi avaa maboksi akipinga combination aliyochaguliwa


Mwanafunzi Josephat John, aliyekuwa anasoma kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Kom iliyopo Manispaa ya Shinyanga, amezua taharuki ya aina yake Mjini Shinyanga mara baada ya kujianika juani huku akiwa amevaa mabango na kujifunika maboksi yenye ujumbe wa kupinga kuchaguliwa masomo ya Economics, Commerce , Accounts (ECA) ambayo amedai hawajawahi kuyasomea kwani yeye amesomea masomo ya Physics, Chemistry, Biology (PCB).

Ametumia mbinu hiyo  ya kuvaa mabango kuiomba Wizara husika ifanye uchaguzi upya wa michepuo ili akasomee masomo ambayo ameshayasoma.

Tukio hili limekuja ikiwa ni siku chache zimepita tangu Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu atangaze matokeo ya wanafunzi waliochaguliwa kwenda vyuo vya ufundi na vyuo vya kati na kidato cha Tano mwaka 2021.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...