Wizara ya Mambo ya ndani ya Iran imemtangaza mhafidhina mwenye msimamo mkali Ebrahim Raisi, kuwa mshindi wa urais baada ya kuhesabiwa kwa kura nyingi na wapinzani kukubali kushindwa.Raisi, mtumishi wa kidini mwenye umri wa miaka 60, anaetajwa kuwa karibu sana na kiongozi wa juu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, atamrithi rais mwenye msimamo wa wastani, Hassan Rouhani.
Hii itaashiria mabadiliko makubwa katika mwelekeo kwa serikali nchini Iran, baada ya miaka minane chini ya Rouhani.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema leo kuwa Raisi amepata kura zisizopungua milioni 17.8, kati ya jumla ya kura milioni 28.6 zilizopigwa siku ya Ijumaa.
Matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutangazwa baadae wikendi hii.
Ebrahim Raisi ataapishwa mwezi Agosti.

No comments:
Post a Comment