Mji mkuu Kinshasa ni kitovu cha maambukizi hayo DRCImage caption: Mji mkuu Kinshasa ni kitovu cha maambukizi hayo DRC
Jamhuri ya Kidemokrasi Congo inakabiliwa na wimbi la tatu la maambukizi ya virusi vya corona, huku mji mkuu Kinshasa ambao ni mji wenye idadi kubwa zaidi ya watu Afrika, ukiwa ni kitovu cha maambukizi hayo, amesema Waziri wa afya Jean-Jacques Mbungani Alhamisi.
Sawa na mataifa mengine ya Afrika, Congo imeripoti maambukizi na vifo vichache, lakini maafisa wa afya wanahofu juu ya ongezeko kubwa la maambukizi ambapo watu 243 walipatikana na Corona Jumatano, kikiwa ni kiwango cha juu zaidi tangu ulipotokea mlipuko mwezi Machi.
"Nilitangaza rasmi mara moja wimbi la tatu la janga la Covid-19 nchini mwetu, Kinshasa kikiwa ni kitovu cha maambukizi," Mbungani aliwaambia waandishi wa habari
Kiwango cha chini cha idadi ya waliochanjwa na kukosa kudumisha usafi ni miongoni wa sababu za kuongezeka kwa kiwango cha maambukizi, alisema.
Kampeni ya chanjo DRC imekwama baada ya kucheleweshwa kuanza kwasababu ya hofu ya usalama wa wa chanjo ya AstraZenecaImage caption: Kampeni ya chanjo DRC imekwama baada ya kucheleweshwa kuanza kwasababu ya hofu ya usalama wa wa chanjo ya AstraZeneca
Jumatano, Shirika la afya duniani (WHO), lilisema lilinahofu juu ya kusambaa kwa aina ya kirusi cha corona cha Delta ambacho kilibainika kwa mara ya kwanza nchini India , ambayo inadhaniwa kuwa ndio inayosambaa zaidi.
Mwishoni mwa juma lililoishia tarehe 30 Mei, kulikuwa na ongezeko la viwango vya maambukizi mjini Kinshasa, WHO imesema
Kampeni ya chanjo DRC imekwama baada ya kucheleweshwa kuanza kwasababu ya hofu ya usalama wa chanjo ya AstraZeneca. Matokeo yake, takriban, 75% ya dozi milioni 1.7 ilizopokea mwezi Machi zilipelekwa katika mataifa mengine ili kuhakikisha zinatumiwa kabla ya muda wake kuisha.
Kwa jumla, Congo imeripoti zaidi ya maambukizi 31,900 na vifo 786 vilivyohusishwa na virusi vya corona tangu janga lilipoanza.
Miongoni mwa wahanga wa corona ni pamoja na wabunge 32, idadi hiyo ikiwa ni sawa na 5% ya jumla ya watu waliouliwa na virusi, maafisa walisema wiki iliyopita.

No comments:
Post a Comment