Search This Blog

Saturday, June 26, 2021

Dawa 101 zaingizwa katika orodha mpya


Serikali ya Tanzania imeongeza dawa mpya katika orodha ya dawa, hatua inayotokana na mabadiliko ya matibabu kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini, Dk Dorothy Gwajima ameyasema hayo leo Ijumaa Juni 24,  2021 wakati akizindua mwongozo wa matibabu nchini na orodha ya Taifa ya dawa muhimu toleo la sita (STG/NEMLIT).

“Baadhi ya dawa zimeongezwa ili kukidhi maboresho ya huduma za kibingwa za kupandikiza figo,” amesema.

Amesema katika kuimarisha huduma za afya ya msingi dawa zimeshushwa katika ngazi ya hospitali za wilaya hadi vituo vya afya ili kuboresha huduma mbalimbali hususani upasuaji.

“Dawa hizo ni pamoja na dawa zinazotumika katika upasuaji na dawa za shinikizo la damu na zile za kutibu ugonjwa wa kisukari,” amesema.

Amebainisha kuwa kwa kuzingatia ushahidi wa kisayansi baadhi ya dawa zimeondolewa katika orodha ya Taifa ya dawa muhimu.

Amesema hiyo ni kwa sababu ama kutokuwa na usalama, ufanisi, ubora wa kutosha au kupatikana kwa dawa nyingine zenye ufanisi zaidi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...