Search This Blog

Sunday, May 2, 2021

Zaidi ya polisi 50 wa Ujerumani wamejeruhiwa katika maandamano ya Mei Mosi

 


Takriban ya maafisa wa polisi 93 wamejeruhiwa na waandamanaji 354 wamekamatwa, baada ya maandamano ya jadi ya Mei Mosi mjini Berlin kugeuka ya vurugu. 

Zaidi ya makundi 20 ya watu yalishiriki maandamano hapo Jana Jumamosi ambapo idadi kubwa wa waandamanaji hao walishiriki kwa amani. 

Lakini maandamano ya mrengo wa kushoto yalioshirikisha kiasi ya watu 8,000 katika mji wa Neukoellin na vitongoji vya Kreuzberg, yaligeuka kuwa ya vurugu. 

Waandamanaji waliwarushia polisi chupa, mawe na kuchoma moto mapipa ya taka na mabenchi ya mbao mitaani. 

Kuna marufuku ya kutoka nje kwa nyakati za usiku katika maeneo mengi ya Ujerumani lakini maandamano ya kisiasa na mikusanyiko ya kidini havimo kwenye marufuku hiyo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...