Mkuu wa ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwenye mazungumzo ya Uingereza kujiondowa kwenye Umoja huo, Michael Barnier, ameonya kwamba ni lazima nchi hiyo itekeleze masharti yote ya kujiondowa, hasa yanayohusika na uvuvi na Ireland ya Kaskazini, ama ipoteze heshima yake kwenye ulimwengu.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini Paris hivi leo, Barnier amesema hadi sasa Uingereza haionekani kuheshimu saini yake iliyoweka kwenye makubaliano ya Oktoba 2019 na kisha tena Disemba 2020.
Wiki iliyopita, boti za wavuvi wa Ufaransa zilizuiwa na meli za jeshi la wanamaji la Uingereza kwenye Mkondo wa Kisiwa cha Jersey, licha ya kuwa makubaliano ya Brexit yaliahidi kuendelea kuwaruhusu kuvua kwenye eneo hilo.
Tayari Umoja wa Ulaya umefunguwa mashitaka dhidi ya Uingereza kwa kuchelewesha kutekeleza makubaliano ya forodha kwa bidhaa zinazowasili Ireland ya Kaskazini kutokea Uingereza.

No comments:
Post a Comment