Rais wa Uganda Yoweri Museveni anaapishwa Jumatano kwa muhula wake wa sita.
Alishinda uchaguzi wa kura iliyozozaniwa mwezi Januari.
Usalama umeongezwa katika mji mkuu, Kampala, kabla ya kuapishwa kwake.
Wakuu wa nchi kadhaa tayari wamewasili kwenye sherehe hiyo - pamoja na kutoka Tanzania, Burundi, Sudan Kusini na Somalia.
Siku ya Jumatatu, polisi walisema zaidi ya watu 40 walikamatwa kwa kupanga kuvuruga sherehe hiyo.
Askari wamezunguka nyumba ya Robert Kyagulanyi maarufu Bobi Wine, ambaye alikuwa mshindi wa pili wa uchaguzi.

No comments:
Post a Comment