Search This Blog

Tuesday, May 11, 2021

Mchezaji wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile afungiwa kucheza mechi tano

 


Mchezaji wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile amefungiwa kucheza mechi tano na kupigwa faini ya Tsh 500,000/= kwa kosa la kutoa maneno ya kejeli, kashfa, udhalilishaji na shutuma dhidi ya Yanga katika mchezo dhidi yao wa 16 bora wa Kombe la ASFC uliyochezwa Uwanja wa Nelson Mandela Rukwa Sumbawanga na Yanga kushinda 1-0.

Taarifa imesema kamati ya mashindano ya TFF ilipitia ripoti mbalimbali ya michezo ya kombe la shirikisho Baada ya kumalizika round ya tano ikiwemo mchezo wa Tanzania Priaon dhidi ya Yanga nakujiridhisha kuwa Asukile ametenda makosa yakutoa maneno ya kashfa kejeli na udhalilishaji dhidi ya timu pinzani, wachezaji wa Yanga na mwamuzi.

Pia kamati imebaini asukile alitoa shutuma za rushwa dhidi ya timu pinzani na shauri hilo limepelekwa kwenye kamati ya maadili ya TFF kwa hatua zaidi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...