Search This Blog

Sunday, May 30, 2021

DR Congo: RaisTshisekedi asema bado kuna kitisho cha mripuko


 Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Felix Tshisekedi amesema hali sio nzuri lakini ipo katika udhibiti baada ya kuripuka kwa volcano katika eneo Goma huko mashariki mwa taifa hilo.

Akizungumza baada ya serikali yake kutangaza kwa makosa kutokea mripuko mwingine wa volkano, ikiwa ni takribani juma moja baada ya mripuko wa Mlima Nyiragongo, Tshisekedi ameonya kwa kusema kwa hali ilivyo mripuko unaweza kutokea kokote katika jiji la Goma kwa kuwataka wakazi wa mji huo kutoharakisha kurejea katika makazi yao.

Taarifa yake hiyo anaitoa baada ya kuwepo kwa ripoti zinazosema zaidi ya wakimbizi 1,000 wameondoka katika kambi walizokuwa wanahifadhiwa huko Rwanda kurejea Goma.

Takribani wakazi 400,000 waliokolewa katika eneo la mashariki la Goma, baada ya wiki moja ya matetemeko ya ardhi, yalitokana na mripuko wa moja ya vokano hai barani Afrika.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...