Takriban watu 11, miongoni mwao watoto wa shule, wameuawa kwa kupigwa risasi katika shule moja katika mji wa Urusi wa Kazan, ripoti zinasema.
Mwalimu mmoja pia alikufa katika tukio hilo kilomita 820 (maili 510) mashariki mwa Moscow.
Watu wawili waliripotiwa kufyatua risasi na mvulana mwenuye umri wa miaka 17 anasemekana kuzuiliwa.
Mlipuko ulisikika na haijulikani ni nini kilitokea kwa mshambuliaji wa pili. Kazan iko katika jamhuri ya Waislamu wengi ya Tatarstan.
Polisi waliojihami vikali na magari ya dharura walionekana nje ya shule hiyo, na video moja katika mitandao ya kijamii ilionyesha watoto wengine wakiruka kutoka madirisha kutoroka pamoja na watu waliojeruhiwa kuhamishwa.
Rais wa Tatarstan Rustam Minnikhanov aliwaambia waandishi wa habari nje ya shule hiyo kuwa ni janga na kwamba watoto 12 na watu wazima wanne walikuwa wakitibiwa hospitalini. "Gaidi huyo amekamatwa. Ana miaka 19. Yeye ni mmiliki wa silaha aliyesajiliwa," alisema.
Video moja kwenye mitandao ya kijamii ilimnasa kijana mmoja akiwa amelala chini akionekana kuzuiliwa nje ya jengo hilo.

No comments:
Post a Comment