Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Blinken ametoa salamu zake za pole kwa kifo cha Prince Philip, mme wa Malkia Elizabeth II, katika mazungumzo ya simu na Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza Raab.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani Ned Price amesema katika taarifa ya maandishi kwamba katika mazungumzo yake na Raab, Blinken alitoa salamu za pole kwa kifo cha Prince Philip aliyefariki akiwa na umri wa miaka 99.
Akibainisha kwamba mawaziri hao wawili walizungumzia suala la Afghanistan, Price alisema,
"Blinken na Raab pia walisisitiza msaada wao kwa Ukraine dhidi ya uchokozi wa Urusi. Mawaziri hao wawili walisisitiza hitaji la Urusi kuachana na mkusanyiko wake wa kijeshi na maneno yake ya uchochezi haraka iwezekanavyo."

No comments:
Post a Comment