Mwanajeshi mweusi wa Marekani mwenye mwenye cheo cha Luteni amewasilisha mashitaka dhidi ya polisi wawili ambao walimshikia bunduki zao na kumpulizia maji ya pilipili wakati alipokuwa akisimamisha magari.
Luteni Caron Nazario amevaa sare yake katika picha iliyochukuliwa na kamera ndogo ya polisi, iliyochukuliwa mwezi Disemba katka jimbo la Virginia.
"Kusema ukweli ninaogopa kutoka nje ," anawaambia maafisa wawili wa polisi. "Yeah unapaswa kuogopa, anasema afisa.
Polisi anasema alisimamishwa kwa kushindwa kuonesha kibali cha kuendesha gari lakini vibali vya muda vinaonekana katika video hiyo.
Katika tukio hilo, mwanajeshi, ambaye alifungwa pingu mikono yake wakati gari lilipokuwa likisakwa , aliuliza ni kwanini nguvu zinatumiwa dhidi yake na akajibiwa na afisa wa polisi: "kwasababu haoneshi ushirikiano." Baadaye aliachiliwa bila mashitaka.
Mashitaka, yaliwasilishwa katika Mhakama ya Wilaya ya Marekani ya Norfolk, Virginia, dhidi ya polisi hao wa idara ya Windsor, Joe Gutierrez and Daniel Crocker, wanaodaiwa kukiukahaki za kikatiba, ikiwa ni pamoja na kushambulia, kufanya msako kinyume cha sheria na kufunga kinyume cha sheria.
Hapakuwa na jibu la moja kwa moja kutoka kwa Idara ya polisi ya Windsor.
Mashitaka haya yanakuja wakatikukiwa na ongezeko la uchunguzi juu ya madai ya ukatili wa posli dhidi ya walio wachache na haki za kijamii.
Afisa wa zamani wa polisi Derek Chauvin kwa sasa anakabiliwa na kesi ya mauaji ya George Floyd.
Picha za Bw Chauvin, ambaye ni mzungu, huku goti lake likiwa limekandamizwa kwenye shingo ya Mmarekani mweusi Bw Floyd ziliibua maandamano makubwa kote duniani dhidiya ubaguzi wa rangi.

No comments:
Post a Comment