Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekaribisha serikali mpya ya mpito la Libya, na kuitaka kuendelea na maandalizi ya uchaguzi mkuu.
Serikali hiyo itachukua nafasi ya ile ya mjini Tripoli inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa, ikiongozwa na waziri mkuu Fayez al-Serraj upande wa magharibi, na ile ya upande wa mashariki yenye mafungamano na mbabe wa kijeshi Khalifa Haftar.
Baraza la Umoja wa Mataifa limesema kuundwa kwa serikali hiyo ya mpito ni hatua ya kihistoria katika mchakato wa kisiasa nchini Libya.
Baraza hilo pia limezitaka pande zote katika mzozo wa Libya kuendelea kuheshimu vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa pamoja na makubaliano ya kusitisha uhasama.
Ijumaa iliyopita, wajumbe kutoka pande hasimu walimchagua Abdul-Hamid Mohammed Dbeibeh kuwa waziri mkuu wa mpito, na Mohammed Menfi kuwa mkuu wa baraza la urais lenye wajumbe watatu.

No comments:
Post a Comment