Wakati Bunge likipitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria uolenga Kiswahili kuwa lugha ya sheria na mahakama, Serikali imewasilisha bungeni Muswada mwingine wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2021 ambao unakwenda kudhibiti usajili wa kampuni nchini.
Muswada huo umesomwa kwa mara ya kwanza bungeni juzi na sasa unakwenda katika kamati kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maoni ya wadau.
Sheria 12 ambazo zinapendekezwa kufanyiwa marekebisho ni Sheria ya Mawakili, Usajili wa Vizazi na Vifo, Majina ya Biashara, Usafiri wa Anga, Sheria ya Makampuni, Usimamizi wa Mazingira na Tafsiri ya Sheria.

No comments:
Post a Comment