Search This Blog

Wednesday, February 17, 2021

JUWAUZA waiomba serikali kutoa elimu juu ya kura za mapema kabla ya kufika uchaguzi


JUMUIYA ya Wanawake wenye ulemavu Zanzibar (JUWAUZA) wameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ), kutoa elimu juu ya kura za mapema kabla ya kufika waati wa uchaguzi kwa lengo la kuondoa sitofahamu kwa wananchi.

JUWAUZA imesema wakati wa uchaguzi Mkuu uliopita mwak 2020 wananchi walikuwa katika hali si ya kawaida kutokana na kutokuwa na eimu yakina juu ya kura za mapema.

Aizungumza na Waandishi wa Habari katika ukumbi wa Jumuiya ya watu wenye ulemavu, (UWZ) Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Salma Haji Saadat alisema kwamba, Juwauza imeona kuwa ipo haja ya Serikali kuongeza juhudi katika kuwaelimsha watu juu ya suala zima la elimu ya mpira kura pamoja n aura za mapema.

“Kutokana na hali iliyokuwa katia uchaguzi uliopia mwaka 2020, kuna haja kubwa ya Serikali kutoa elimu ya mpiga kura mapema kwa wananchi a kuwafahamisha namna ya umuhmu wa kura za mapema ili kuonda mkanganyio baina yao,” alisema.

Bi. Saadat alisema, licha ya uwepo kwa vikundi mbalimbali ambavyo vilikuw vnaelimisha juu ya kura za mapema bad kuna wimbi kubwa la watu waishio vijijini elimu hiyo haikuwafika.

Alifafanua kuwa njia zilikuwa zintumia ni redio na televisheni hivyo na kufay baadhi ya watu wengi kutofiki hivyo aliishauri serikali kubuni mbinu mbadala na ya mapema ya kufikisha elimu ya mpiga kura kwa urahisi kwa wanchi wote.

“Kuna makundi amayo hayafikiwi na elimu hii ya mpiga kura, hawaju hata hiyo kura ya mapema ni nini hiyo Serikali ibuni njia ambao itatumika katika kuwaelimisha wananchi hususani makundi aaalumu wakiwemo watu wenye ulemavu,” alifafnua.

Akitoa tathmini ya uchaguzi mkuu uliopita Bi. Salma Saadat alisema kwamba, katika uchaguzi uliopita hakukuwa na mazingira ambayo ni rafiki kwa watu wenye ulemvu na kuwafanya kushindwa kushiriki mchakat mzima wa kampeni n ahata hatua ya upigaji wa kura.

“Katika kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020, waangalizi kutoka JUWAUZA tulibaini  mapungufu kadhaa ambapo mazingira hayakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu, kama vile maeneo ya viwanja vya kampeni na sehemu za kupigia kura watu wenye ulemavu wa ngozi walishindwa kpata kivuli na ushiriki mihkat hiyo,” alieleza

Hata hivyo alieleza kwamba katika mchakato mzima wa uchaguzi mkuu hakukuwa na wakalimani wa uha za alama ambapo kundi kubwa la watu wenye ulemavu walishindwa kufuatilia kampeni.

“Jambo jingine ambalo tulilibaini wakati wa kampeni, katika mikutano ya Siasa maegesho ya gari yalikuwa mbali sana lakini sehemu hazikuwa rafiki kwa watu wenye elemavu,” alifafanua.

Sambamba na hayo Salma Saadati alieleza kuwa Tume ya Uchaguzi Zanzibar iapaswa kufaya kazi na vyama vya Siasa ili kushinikiza kwa Serikali juu ya uumuishaji wa wanawake na watu wenye ulemavu kuingia katika king’anyiro cha kugombea nafasi mbalimbali.

Mkutano wa Waandishi wa Habari na Mwenyeiti huyo wa Jumuiya ya wanawake walemavu (JUWAUZA) ulikuwa nan a lengo la kutoa ripoti yenye tathmini nzima ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 juu ya watu wenye ulemavu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...