Na Faruku Ngonyani , Mtwara.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Gelasius Byankwa amemuomba katibu Mkuu wa baraza la mitahani Tanzania (NECTA) DKT. Msonde kukanusha taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayoonesha shule kumi za mwisho ya matokeo ya kidato nne kutoka Mtwara.
Byankwa amesema kuwa kwa taarifa ya matokeo yaliyotolewa na baraza la Mitihani yenye kurasa 21 haina kipengele kinachoonesha shule kumi za mwisho kitaifa.
Hivyo ameliomba baraza hilo kuptia kwa katibu mkuu wake kukanusha taarifa hizo huku taarifa za awalizimeonesha katibu Mkuu kupitia baraza hilo ameahidi kukunusha taarifa muda wowote kutoka sasa.
Lakini pia Mkuu huyo wa Mkoa mezungumzaia juu ya matokeo hayo kwa ujumla ambapo kwa darasa la nne kwenye Halmashauri kumi zilizofanya vizuri Mtwara imetoa halmashsuri ya wilaya ya Newala,kidato cha katika halmashsuri kumi zilizoongeza ufaulu vizuri ipo Newala na Tndahimba huku kidato cha nne Halmashauri Manispaa Mtwara Mikindani imeshika nafasi ya Tisa(9) katika halmashauri zote zilizopo nchini.
Aidha Mkuu Mkoa amechukua fursa hiyo kuwasihi wananchi kuacha kusambasa taarifa ambaso hazijahaikikiwa kwa kuwa kufanya hivyo ni kikuka sheria ya mitandao hapa nchimi.

No comments:
Post a Comment