Search This Blog

Thursday, December 24, 2020

Tetesi za soka kimataifa


Chelsea imejiunga katika kinyang'anyiro cha kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Erling Braut Haaland, 20, lakini Manchester City inajichukulia kuwa ndio ilio kifua mbele kumsajili mchezaji huyo.. (90 min)

Matumaini ya Manchester United katika kumsajili Halaand huenda yakadhoofishwa kutokana na uhusiano wake na wakala Mino Raiola, ikimaanisha kwamba mshambuliji wa Everton Dominic Calvert-Lewin, 23, huenda akawa mbadala wa kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer. (Mirror)

Chelsea ina mpango wa kutoa fedha za kumsajili Haaland, na kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice kupitia kuwauza wachezaji saba Ross Barkley, 27, Mhispania Marcos Alonso, 29, Mjerumani Antonio Rudiger, 27, rias wa Denmark Andreas Christensen, 24,mchezaji wa Itali Jorginho, 29, raia wa England Danny Drinkwater, 30, na mchezaji wa Nigeria Victor Moses, 30. (Sky Sports via the Sun)

Paris St-Germain inamnyatia Rudiger, huku beki huyo akipata tatizo la kujiunga na kikosi cha kwanza katika klabu ya Stamford Bridge. (Le Parisien - in French & subscription required)

Liverpool ina hamu ya kumsajili beki wa Real Madrid na Eder Militao, 22, huku mchezaji huru wa Argentina Ezequiel Garay, 34, akitarajiwa kujiunga na klabu ya Jurgen Klopp. (Todofichajes - in Spanish)

Mikael Arteta na Arsenal Arsenal wana hamu ya kumsaini mshambuliaji wa Real Madrid na Brazil Vinicius Jr, 20, kwa mkopo mwezi Januari , lakini wameamua dhidi ya kumsaini mchezaji mwenza na kiungo wa kati wa Uhispania Isco, 28, ambaye anatarajiwa kujiunga na Juventus. (Daily Star)

Barcelona imeanza mazungumzo na beki wa Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi, 28, ya uhamisho wa bila malipo wakati kandarasi yake itakapokamilika mwisho wa msimu. (SPOX via 90 min).

Mkufunzi wa klabu ya Derby county Wayne Rooney anataka kumsaini belikuwa mchezaji wa Man United na England Phil Jones, 28, kuwa mchezaji wake wa kwanza kumsajili katika timu hiyo ijapokua Rams huenda ikakabiliwa na ushindani kutoka kwa West Brom na Burnley. (Metro)

Everton na Wolves wanatarajiwa kukabiliana na AC Milan katika kumsajili beki wa Strasbourg na Ufaransa Mohamed Simakan, 20, ambaye anapatikana kwa dau la £20 million. (Tutto Mercato Web - in Italian

Kipa Loris Karius, 27, huenda akarudi katika klabu yake ya Liverpool , baada ya Union Berlin kufikiria kusitisha kandarasi yake mapema huku mchezaji hyo wa Ujerumani akichezeshwa mara moja tangu kuanza kwa msimu. (Kicker via The Sun)

Barcelona inajaribu kumrai kiungo wa kati wa Uhispania Ruqui Puig kutia saini kandarsi mpya , lakini huku kuondoka kwake kukitarajiwa Manchester City na Bayern Munich zote zinamtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Fichajes - in Spanish)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...