Search This Blog

Monday, December 28, 2020

Mawaziri wa Libya na Misri wajadili ushirikiano


Waziri wa Mambo ya Nje wa Libya Mohammed Tahir Siyala alijadili suala la ushirikiano na utulivu wa Libya na Waziri mwenzie wa Misri, Samih Shukri.

Katika taarifa iliyoandikwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Libya, ilielezwa kuwa Siyala na Shukri walizungumza kwa njia ya simu.

Katika taarifa hiyo, ilielezwa kuwa wawili hao walijadili hali ya hivi karibuni nchini Libya na kuzungumzia ushirikiano kwa ajili ya kudumisha hali ya utulivu.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Libya Fethi Bashagha alikutana na wajumbe kutoka Misri hapo jana katika mji mkuu Tripoli, na kujadili masuala ya pamoja ya kuendeleza ushirikiano wa usalama kati ya nchi hizo mbili.

Ilibainika pia kuwa mkutano huo ulijadili kuungwa mkono kwa makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya vyama vya Libya na matokeo ya mikutano ya 5 + 5 ya Kamati ya Pamoja ya Jeshi iliyofanyika Geneva, Uswizi mnamo 19-23 Oktoba.

Ilielezwa kuwa mkutano husika ulifanyika katika mfumo wa sera za usalama za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya, ambazo zinalenga kukuza ushirikiano na nchi jirani na kuzingatia umuhimu wa hatua ya pamoja kati ya utawala wa Cairo na Tripoli.

Kama matokeo ya mikutano ya 5+5 ya Kamati ya Pamoja ya Jeshi iliyofanyika Geneva, Uswizi, mnamo Oktoba 19-23, makubaliano ya kudumu ya kusitisha vita yalitiwa saini kati ya serikali ya Libya na wajumbe kutoka vikosi vya Khalifa Haftar.

Mnamo Desemba 19 katika mji wa Benghazi, Abbas Kamil ambaye ni mkuu wa Idara ya Ujasusi ya Misri, alikutana na Khalifa Haftar ambaye ni kiongozi wa vikosi haramu vinavyoendesha harakati mashariki mwa nchi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...