Search This Blog

Saturday, December 19, 2020

Barnaba Classic afunguka kutomsaidia baba yake



Msanii Barnaba Classic amenyoosha maelezo kufuatia video clip inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii ikimuonyesha baba yake mzazi akilalamika kwamba anapata shida na hapati msaada kutoka kwa mwanaye

Akijibu kuhusiana na hilo Barnaba Classic amesema yule ni baba yake mzazi ila anachokiamini hana tatizo lolote na baba yake japo alikuwa hajui kinachoendelea.

"Yule ni baba yangu mzazi kabisa wala sio jambo la kiki , waswahili wanasema mzazi hakosei, hasemwi na hakosolewi, ukiachana na hayo mnayoyasikia mimi sina tofauti wala matatizo na baba yangu, namshukuru Mungu kwa kila jambo ila sitaki kulizungumzia sana suala hili nilikuwa sijui kinachoendelea" amesema Barnaba Classic 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...