Search This Blog

Tuesday, November 17, 2020

Tetesi za soka kimataifa

 


Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli amefanya mazungumzo na timu ya Championi ya Barnsley. Muitalia huyo mwenye umri wa miaka 30 , yuko huru baada ya mkataba wake na Bresica kusitishwa kwa kutohudhuria mazoezi . (Sun)

Chelsea wanataka kusaini mkataba na kiungo wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 17 badala ya kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 21. (Eurosport)

Leicester wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa safu ya nyuma -kushoto Mreno Nuno Mendes, 18, ambaye anakipengele cha kumnunua cha pauni milioni 40 katika mkataba wake na Sporting Lisbon. (Mail)

Kiungo wa kati wa zamani wa Juventus midfielder Claudio Marchiso amemtaka mchezaji wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 27, arejee katika klabu hiyo ya Italia . (Mirror)

United watapatia kipaumbele mauzo ya wachezaji mwezi wa Januari huku mlinzi wa England Phil Jones, 28, na Waagerntina mlinda lango Sergio Romero, 33, na beki Marcos Rojo,30, wakiwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo. (Manchester Evening News)

Mazungumzo ya mkataba wa Watford na winga Adama Traore yamekwama kwasababu Muhispania huyo hafurahii muda anaopewa kucheza gemu . Kijana huyo mwenye umri wa miaka 24 awali alihusishwa na taarifa za kuhamia Barcelona. (Goal)

West Ham wamepewa ofa ya kusaini mkataba na mshambuliaji wa Real Mdrid Muhispania Mariano Diaz, 27.

Arsenal wanaangalia uwezekano wa kufanya mkataba wa kubadilishana wachezaji na Inter Milan ambao utamuwezesha Mdenmark na mlinzi wa zamani wa Tottenham Christian Eriksen, 28, kujiunga na the Gunners na kiungo wa kati Mswiss Granit Xhaka, 28, kuhamia katika klabu hiyo ya Italia . (Corriere dello Sport, via Talksport)

Meneja wa zamani wa Chelsea Antonio Conte anasema alitaka kusaini mkataba na mlinzi wa Liverpool Virgil van Dijk na Romelu Lukaku wa Inter Milan wakati alipokuwa katika klabu hiyo . (Telegraph)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ufaransa Olivier Giroud, 34, atakwenda mapumzikoni mwezi Januari kama muda wake wa kucheza hautaongezwa katika kipindi cha miezi ijayo . (The Athletic - subscription retired)

Arsenal hawatamsaini Mitchel Bergkamp - mtoto wa kiume wa mchezaji wa zamani wa Gunners Dennis Bergkamp - licha ya kwamba Muholanzi huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akifanyiwa majaribio ya kimchezo kwa wiki moja katika klabu hiyo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...