Search This Blog

Monday, August 17, 2020

Dkt. Bashiru watia nia wa ubune kubaki kwenye majimbo yao

 

KATIBU Mkuu wa CCM, Dk. Ali Bashiru  amewataka wote waliotia nia kugombea ubunge


kubaki kwenye majimbo yao kusubiri majina yatakayopitishwa na Halmashauri Kuu


ya chama hicho inayokaa Dodoma Agosti 20, 2020.


Dk. Bashiru amesema inabidi wabaki kwenye majimbo yao


ili iwe rahisi kwa watakaopitishwa kugombea, kwenda kuchukua fomu, kutafuta


wadhamini na kurejesha fomu ili Agosti 25 mwaka huu wazirejeshe Tume ya Taifa


ya Uchaguzi kwa ajili ya uteuzi.


Ameyazungumza leo baada ya kuzindua Kituo cha CCM CHA Mawasiliano ya Habari za Uchaguzi Mkuu wa Tanzania ambao kampeni zake zinatarajia kuanza mwishoni mwa mwezi huu.


Amesema kuwa leo kimekaa kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri


Kuu ya Taifa, kuandaa taarifa ya wagombea itakayopelekwa kesho katika kikao


cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuchuja majina kwa mujibu wa katiba


ya chama hicho na hatimaye kuyapeleka Halmashauri Kuu Agosti 20 itakayoteua


jina moja la mgombea kwa kila jimbo na wagombea wa viti maalumu.


“Kazi ya Sekretarieti siyo kufanya uteuzi bali ni kuandaa


nyaraka, kufanya uchambuzi  taarifa  za vikao vya wilaya na mikoa za watia nia


ubunge na wa viti maalumu ngazi ya Taifa, tunachambua na kuandaa mapendekezo na


kuvipeleka Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa  na hatimaye 


Halmashauri Kuu ya Taifa kwa aijili ya uteuzi.” Amesema na kuongeza


kuwa…


“Tunarajia sifa za chama chetu ndiyo msingi mkubwa, na chama


chetu kwa sifa zake tutakuwa pia na viongozi wenye sifa hizo, kwa hiyo sifa za


viongozi wanaotakiwa zipo kwenye Katiba na kanuni za uteuzi , mwadilifu, mchapakazi,


jasiri, mzalendo, msikivu kwa anaowaongoza, mwenye nidhamu ya kutii maelekezo


ya vikao wa chama.”


Amesema kuwa anatatarajia katika waliotia nia  kugombea zaidi 10,000,  kati yao watapata  wagombea bora, kwa sababu ya kipimo cha chama


ni kuwa na hazina ya  viongozi, ni idadi


ya waliotia nia na kwamba  mchakato


umekuwa wazi kwa nchi nzima, kwenye urais, ubunge na udiwani. Kuhusu


wawakilishi utaratibu wake utafanyika baadaye kwani  ratiba ya uchaguzi na kampeni imekuwa tofauti


kwa Zanzibar.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...