Search This Blog

Saturday, July 11, 2020

Waathirika wa mafuriko wapatiwa msaada


Kaya 1800 zilizopo katika kijiji cha Mbuchi Tarafa ya Mbwera wilayani Kibiti Mkoani Pwani ambazo zimeathirika na Mafuriko Makubwa yaliotokea Mwezi March Mwaka huu zimepatiwa Msaada wa tani 15 za Vyakula ili kuwasadia wakati wakijiandaa na Shunguli zao za Kilimo.

Wananchi hao wanaoishi katika Delta ya Mto rufiji walipoteza vyakula,uharibifu wa Mashamba na nyumba kutokana na Mvua kubwa zilizokuwa zikinyesha lakini pia kutapika kwa Maji kutoka katika Mto ruaha na kusababisha mafuriko makubwa katika Maeneo yao.

Taasisi ya Kimataifa ya Misaada ya Kiislam Direct Aid imetoa Tani 15 za Vyakula, mafuta na sukari kwa ajili ya Kuwasaidia wananchi hao ambao wanajishughulisha na Shughuli za Kilimo na Uvuvi.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...