Search This Blog

Sunday, July 19, 2020

Shamkhani amwambia Pompeo: Kukiri kushindwa na Iran ni bora kuliko bwabwaja za kijinga


Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran amejibu madai ya Mike Pompeo Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani na kusema kuwa, ni bora Washington ikiri kwamba, imeshindwa na Iran badala ya viongozi wake kuendelea na bwabwaja za kijinga.
Ali Shamkhani ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter akimhutubu Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani kwamba, zaidi ya miaka 40 sasa serikali ya Washington imetumia nguvu zake zote ili itoe pigo kwa Iran lakini imekwama na kushindwa kufikia malengo yake.
Shamkhani amesema kuwa, kukiri kushindwa mbele ya Iran yenye nguvu na imara ni bora kuliko kuendelea kutoa matamshi ya uropokaji wa kijinga.

Jibu hilo la Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran linafuatia madai ya Mike Pompeo, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani aliyesema kuwa, ili kukabiliana nja nchi mfano wa Iran ni kutumia nguvu ntu ndiko kunakofaa na si vinginevyo.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, wachambuzi wengi wa masuala ya kisiasa hata wa ndani ya Marekani kwenyewe wamekuwa wakikiri hadharani kwamba, siasa za vikwazo, vitisho na mashinikizo za serikali ya Washington dhidi ya Iran zimefeli na kugonga ukuta kwani hazijaweza kabisa kuifanya Tehran isalimu amri na kufuata matakwa ya dola hilo la Magharibi.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...