Search This Blog
Sunday, July 26, 2020
CCM kata ya Mpiruka wamuamini Issa Makota awe mgombea wao wa udiwani
Na Ahmad Mmow, Nachingwea.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) kata ya Mpiruka leo wamemchagua Issa Makota apeperushe bendera ya chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020 kwa nafasi ya udiwani wa kata ya Mpiruka, halmashauri ya wilaya ya Nachingwea.
Issa Makota ambae ni askari mstahafu wa jeshi la polisi amejinyakulia kura 30 kati ya 81 za wajumbe wote waliohudhuria mkutano huo.
Makota alifuatwa kwambali na Thimetheo Godfrey aliyepata kura 16 kati ya hizo 81.
Aliyekuwa diwani wa kata hiyo mwaka 2015 kupitia CCM, Hamis Ngajupa amepata kura 15, sawa na Bakari Kinunda Rwaba ambaye pia amepata idadi kama hiyo.
Aidha diwani aliyemaliza muda wake, Jamal Tamba ambaye alikuwa diwani wa kata hiyo kupitia Chama cha Demokrasia Maendeleo ( CHADEMA) na baadae kumtimkia CCM ameambulia kura mbili ambazo zinalinganana alizopata Bonaventura Chembe.
Jaribu Zuberi Chakiwe ambae nae pia alijaribu bahati yake katika kura hizo za maoni amejipatia kura moja. Huku George Damla Milanzi akiondoka mikono mitupu.
Matokeo ya ya wagombea kata nyingine na kata zao kwenye mabano hadi habari hii inaandikwa ni Said Hawdh ''Saala'' (Nachingwea), Saada Makota( Mkotokuyana), Ali Chitanda( Nangowe), Said Makayola( Ngunichile), Napepa( Boma), Ahmad Makoroganya(Ugawaji) na Chimbonaga A( Naipanga).
Wengine ni Abdallah Nkane(Nditi), Simon Mkwalila(Nang'ondo), Michinge Mchopa(Kilimanihewa), Adnani Mpyagila(Mbondo), Ramdhan Mpilipili( Stesheni) na Monica Kasembe(Nambambo).
Pia wamo Slyvanus Chembe(Naipingo), Joyce Ntauka(Ruponda), Seleman Katali(Marambo) na Edward Mhagama (Namikango).
Wilaya ya Nachingwea iliyopo mkoa wa Lindi ina kata 36. Ambapo hadi sasa baadhi kata, matokeo yake ya kura za maoni hayajapatikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment