Search This Blog

Sunday, June 14, 2020

SIPRI: Nchi zenye silaha za nyuklia zaendelea kuziimarisha


Taasisi ya SIPRI imesema idadi ya vichwa vya nyuklia imepungua hadi 13,400 mwa mwaka huu. Lakini nchi tisa zenye silaha za kinyuklia zinazidi kuziimarisha kuwa za kisasa zaidi.

   
Kwenye ripoti yake iliyotolewa leo Jumatatu, taasisi hiyo ya kimataifa ya utafiti wa amani na pia inayofuatilia biashara ya silaha (SIPRI) imesema kuwa kiujumla idadi ya vichwa vya nyuklia ilipungua ulimwenguni kwa 465 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka wa 2019.

Takwimu hiyo ilijumuisha vichwa vya nyuklia ambavyo vimeshaunganishwa kwenye makombora, ambavyo vimehifadhiwa pamoja na vinavyopaswa kukongolewa au kuharibiwa.

Kupungua kwa idadi hiyo kumetokana na kukongolewa kwa vichwa vya nyuklia vya zamani vya Urusi na Marekani.

Kwa pamoja mataifa hayo mawili yanamiliki asilimia 90 ya silaha zote za kinyuklia ulimwenguni.

SIPRI imekadiria kuwa Marekani inavyo vichwa vya nyuklia 5,800 huku Urusi ikiwa na vichwa 6,275 vya nyuklia.

Uingereza, Ufaransa, China, India, Pakistan, Israel na Korea Kaskazini ni miongoni mwa nchi ambazo zimetajwa kumiliki silaha za nyuklia.


Taasisi ya SIPRI imekadiria kuwa Uingereza ina vichwa vya nyuklia 215, Ufaransa inavyo 290, China 320, India 150, Pakistan 160 na Israel 90. Korea ya Kaskazini inaaminika kumiliki kati ya vichwa 30 hadi 40, lakini havikujumuishwa kwenye makadirio ya taasisi ya SIPRI kuhusu idadi jumla ya vichwa vya nyuklia ulimwenguni.

SIPRI imesema kuwa takriban vichwa vya nyuklia 1,800 vimewekwa katika hali ya kuwa tayari sana kwa matumizi.

Marekani na Urusi zinaongoza katika umiliki wa silaha ya nyuklia ulimwenguni: SIPRI

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...