Search This Blog

Sunday, June 14, 2020

OSHA watakiwa kusimamia sheria ya usalama mahala pa kazi


Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) umetakiwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Afya na Usalama Mahali pa Kazi ikiwemo kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya Usalama na Afya kazini ili kupunguza ajali na magonjwa yanayoweza kutokea katika sehemu za kazi.

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Andrew Massawe, alipotembelea ofisi za OSHA kwa ajili ya kufuatilia utekelezaji wa maagizo mbalimbali ya kiutendaji ambayo aliyatoa kwa viongozi wa taasisi hiyo mwezi Januari mwaka huu.

Aidha, Bw. Massawe ameeleza kuridhishwa kwake na utekelezaji wa maagizo yake ikiwemo kuanzishwa kwa mfumo wa kieletroniki wa usajili na usimamizi wa sehemu za kazi (WIMS) na programu mbalimbali za kuelimisha wananchi pamoja na kuboresha tovuti.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...