
LONDON, ENGLAND . SUPASTAA, Wilfried Zaha ametumia ipasavyo mapumziko yake baada ya kumchukua mpenzi wake, mrembo Paige Bannister na kwenda kula naye raha huko Barbados.
Crystal Palace kwa sasa haina mechi, hivyo jambo hilo limemfanya Zaha kutumia fursa ya kusafiri kwenda kupumzika na kipenzi cha moto wake huko visiwa vya Caribbean.
Mapumziko hayo yamekuja wakati mwafaka kwa staa huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, kwa sababu alipata nafasi ya kuwa na mpenzi wake karibu wakiponda raha katika Siku ya Wapendanao.
Zaha amekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mrembo Paige tangu mwaka 2016 na hilo lilijulikana baada ya kuonekana pamoja huko Wembley.
Zaha hakutaka kuwanyima mashabiki wake fursa ya kuona kile alichokuwa akifanya na mpenzi wake baada ya kuamua kuposti pocha za matukio kwenye ukurasa wake wa Instagram.
Zaha atarudi uwanjani kupiga mzigo Jumamosi ijayo wakati watakapokipiga na Newcastle United, alisema pia kwamba anapiga bata, lakini amekuwa akikumbuka kujitolea kwa jamii akisema:"Natoa fungu la 10 la mshahara wangu kuchangia kila mwezi, hivyo kwenye hilo najitahidi kwa kadri ya uwezo wangu. Mama yangu anahakikisha kila mwisho wa mwezi unapofika, nafanya kila kitu kusaidia.”
No comments:
Post a Comment