Search This Blog

Sunday, February 2, 2020

Maskini Samatta Alia na Watanzania “Naomba Muache Kutoa Maneno Mabaya Kwenye Ukurasa wa Timu Yetu, Sifurahishwi”


Mchezaji wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Aston Villa Mbwana Ally Samatta amelia na Watanzania kwa kuwaomba waache kutoa maneno mabaya kwenye ukurasa wa timu yake ya Aston Villa.

Hii inakuja baada ya Watanzaia wengi kulalamika kuwa Samatta ananyimwa pasi na wachezaji wa klabu hiyo .

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Samatta ameandika ujumbe huu:-

“Mashabiki wa soka Tanzania nafaham kuwa mnanipenda kijana wenu na mnapenda nifanye vzr ktk timu yangu mpya,lakini nawaomba muache kutoa maneno ya kashfa au yenye mlengo mbaya katika ac/ za timu au wachezaji, binafsi sifurahishwi.”


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...