Search This Blog

Sunday, January 26, 2020

Solskjaer kuletewa mastaa sita wapya Manchester United

Manchester, England. KOCHA wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer bado anakingiwa kifua na bodi na kwamba atasajiliwa wachezaji sita wapya ili kuokoa kibarua chake.
Kocha huyo atapewa nguvu kwenye kufanya usajili wakati klabu ikimhitaji kubadili hali ya mambo ya kuifanya timu kuwa imara tena.
Solskjaer mwenyewe alisema kwamba anaamini timu itamvumilia na kumpa muda wa kuitumikia timu hiyo kama Liverpool walivyofanya kwa Jurgen Klopp.
Makamu mwenyekiti wa Man United, Ed Woodward anatazamiwa kumpa Solskjaer bajeti ya kutosha ya kufanya usajili ili kurekebisha mambo kwenye kikosi hicho kinachoonekana kuwa na shida nyingi.
Kocha huyo ameambiwa kwamba atahitaji zaidi ya vipindi viwili vya usajili ili kujenga kikosi kitakachokuwa kwenye uwiano mzuri.
Kikosi cha Man United kilichochapwa na Burnley kiliundwa na wachezaji waliosajiliwa na makocha watano tofauti kuanzia kwa Sir Alex Ferguson.
Wachezaji wa Solskjaer walikuwa watatu tu, Aaron Wan-Bissaka (Pauni 50 milioni), Harry Maguire (Pauni 85milioni) na Daniel James (Pauni 15milioni).
Na sasa kocha huyo atapewa fursa ya kusajili beki wa pembeni upande kushoto ambapo kuna mastaa kama Ben Chilwell na David Alaba wanapewa nafasi huku kwenye kiungo ya kati watanaswa wawili, Matias Vecino na pengine Ivan Rakitic na watahitaji namba 10 mmoja, ambapo hapo orodha ya mastaa wanaosakwa ni James Maddison, Bruno Fernandes, Philippe Coutinho na Christian Eriksen.
Mchezaji mwingine wanayemsaka kwenye nafasi hiyo ni Jack Grealish wa Aston Villa.
Man United itaingia sokoni pia kusaka winga mmoja, ambapo mkali Jadon Sancho amekuwa akitajwa kwenye hilo ili kuungana na wakali wengine huko Old Trafford huku wanasaka straika mmoja ambapo orodha  inawahusu Moussa Dembele na Lautaro Martinez.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...