Search This Blog

Thursday, January 23, 2020

Mabeste "PESA Imevunja Ndoa Yangu...Alikuwa Akisafiri Kumbe Analala Kwa Jamaa Yake"

Mabeste asema Ndoa yake imevunjika sababu Lisa alikuwa akimsaliti kwa kuchepuka, Pia kutokuwa na pesa kulimfanya Lisa atake waachane

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, Mabeste amesema kuwa mzazi mwenziye ndiyo aliyeanza kumwambia kwamba waachane, jambo ambalo limemuumiza sana.

"Mimi na yeye tulikata hizo stori tangu mwaka jana, tulikuwa hatuongei na hata watoto hajawahi kuniletea niwaone nikimtumia ujumbe kuhusu familia yangu hanijibu, alinifata akaniambia tuachane nikakubali, mtu ambaye ameenda kuishi naye ni rafiki yangu ambaye tunafanya kazi" amesema Mabeste.

Aidha Mabeste ameendelea kusema "Siwezi kumtaja huyo rafiki yangu anayeishi naye kwa sasa ila ni muongozaji wa video 'Director', nilikuwa namuuliza kitu gani kinaendelea anakataa, mke wangu nilimpa uhuru sana, kumbe alikuwa akitoka Moshi kuja Dar analala kwa jamaa, mimi ananidanganya kwamba yupo kwa dada yake" ameongeza.

Cha mwisho amesema alichokigundua hadi imesababisha kuachana kwao ni kutokuwa na pesa za kutosha.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...