Search This Blog

Sunday, November 3, 2019

Mamia ya Wasafiri wamekwama baada ya Bomba la Gesi Kupasuka Kilwa,Lindi


Mamia ya Wasafiri wamekwama kwa saa zaidi ya 3 karibu na eneo la kati ya Songas na Banduka, Wilaya ya Kilwa Lindi baada ya bomba la gesi kwenye mitambo ya umeme kudaiwa kupasuka, Polisi wamezuia magari na vyombo vingine vya moto kupita eneo hilo ili kuepusha madhara.

Gesi hiyo inavuja kwenye kituo hicho kinachomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) hivyo kuwashawishi walinzi wa kituo jirani cha kupokea gesi kutoka Madimba Mtwara na Songosongo kilicho chini ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kusaidia kuimarisha ulinzi.

“Ni kweli kuna hitilafu kidogo. Wataalamu wetu wanashughulikia hali hiyo ila hakuna moto wala madhara yoyote kwa binadamu,” amesema Nigel Whittaker mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Songas.

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...