Search This Blog

Friday, November 22, 2019

Emery afanya mpango Xhaka asihame

LONDON, ENGLAND . KOCHA, Unai Emery anaamini kwamba atamshawishi kiungo wake Granit Xhaka aachane na uamuzi wa kuachana na kikosi cha Arsenal kwenye dirisha la Januari.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Uswisi, Xhaka amekuwa hana furaha tangu alipovuliwa unahodha kwenye kikosi hicho baada ya kutibuana na mashabiki wa Arsenal wiki nne zilizopita. Jambo hilo lilimfanya aondoshwe kwenye kikosi katika mechi nne zilizopita tangu tukio hilo la mashabiki lilipotokea kwenye sare ya 2-2 dhidi ya Crystal Palace.
Wakati akiwa kwenye mechi za kimataifa, Xhaka alisema: “Ninafahamu namna gani ya kuendelea na mambo yangu kwa sababu sikukubaliana kabisa na kilichotokea.”
Wakati kikosi hicho cha Arsenal kikijiandaa kuwakabili Southampton leo Jumamosi, kocha Emery anaamini kwamba kiungo wake huyo atakuwa fiti kurejea kwenye kikosi. Lakini, kocha huyo alisema kitu cha kwanza Xhaka anachopaswa kufanya ni kumalizana na mashabiki wa timu hiyo.
“Kwenye mazoezi alifanya vizuri na nilizungumza na Granit anataka kurudi kwenye timu. Anaendelea vizuri na anaamini timu yake ni Arsenal," alisema Emery akimzungumzia kiungo huyo.
Xhaka, ambaye alinaswa kwa Pauni 38.25 milioni kutoka Borussia Moenchengladbach mwaka 2016, mkataba wake bado umebakiza miaka miwili na nusu huku akilipwa Pauni 100,000 kwa wiki. Kulikuwa na taarifa kwamba Inter na AC Milan zimeweka wazi mpango wa kupeleka ofa ya kumsajili staa huyo kwenye dirisha la Januari huku kukiwa na timu kadhaa za Ujerumani. Xhaka alicheza mechi zote za Uswisi za kufuzu Euro 2020 dhidi ya Georgia na Gibraltar wiki iliyopita, lakini haonekani kama atapangwa kwenye mchezo wa Arsenal dhidi ya Southampton huko Emirates leo Jumamosi.

Let's block ads! (Why?)

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...