Search This Blog
Wednesday, November 13, 2019
Diamond Platnumz na Mbwana Samatta wanastahili kutunukiwa PhD ya heshima
Niende kwenye mada moja kwa moja.
Kwa msanii kama Wizkid na Tiwa Savage kuja Tanzania, kualikwa na mtoto wa Tandale, mtoto alielelewa na single mother kwa maisha ya kubangaiza, mtoto ambaye hata Form 4 hajamaliza kama kamaliza basi kafeli) ni bonge la achievement.
KiukwelI Diamond kaleta mabadiliko makubwa mno na anastahili sanamu lake liwekwe pale mjini posta,na kumbukumbu zake ziwekwe makumbusho ya taifa, apewe hata PhD ya heshima akiwa hai tusisubiri afe ndo tuanze unafiki! Leo hii Diamond ameajiri watu zaidi ya 200, wenye elimu kumzidi na wasio na elimu. Watanzania tuweke unafiki na ushabiki pembeni, tuanze ku- appreciate vya kwetu.
Pia kuna mtu kama Samatta (SamaGoal), naye anastahili heshima ya PhD na sanamu lake liwekwe pale nje Uwanja wa Taifa.
Wapo wengi sana walioleta mabadiliko kwa nchi yetu tuwaenzi hawa ma living legends wetu tusisubiri wafe ndio tuanze UNAFIKI!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment