Search This Blog
Thursday, October 24, 2019
Rais Magufuli alinipigia simu saa 10 usiku, nikasikia sauti usingizi wote ukakata - Harmonize
Na. Emmy Mwaipopo, Dar
Msanii wa Muziki, Harmonize amesema baada ya wimbo wa 'Magufuli' kutoka Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli alishawahi kumpigia simu saa 10 usiku na aliposikia sauti usingizi wote ukakatika.
Harmnize amesema kuwa Rais Magufuli alimshukuru sana na kumwambia wimbo alioutoa unajenga mtu hata mtu akiwa kijijini huko akiuona anaona maendeleo kwasababu katika wimbo huo ameonyesha kila kitu.
"Baada ya wimbo kutoka nakumbuka Rais Magufuli alishawahi kunipigia simu usiku ilikuwa mida ya saa 10 hivi, nimetoka zangu kurekodi niko zangu nyumbani nikasikia sauti nikashtuka usingizi wote ukakatika akaniambia bwana nashukuru sana wimbo wako unajenga nchi unajua maendeleo yapo na yanafanyika," amesema Harmonize.
"Unajua mtu kama yuko Singida umwambie Dar es Salaam kuna Airport hajui lakini kwenye ile nyimbo umeelezea kila kitu na umeonyesha umemfanya hadi mtu wa Sumbawanga, Shinyanga kumbe serikali ya Awamu ya Tano inafanya kazi so akaniambia hongera sana wimbo wako unajenga taifa kiukweli."
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment