Search This Blog

Monday, September 16, 2019

Rais Magufuli azuia ukusaji mapato machinjio ya Vingunguti


Rais John Magufuli ameuagiza uongozi wa Hamashauri ya Ilala kutochangisha fedha katika machinjio ya Vingunguti hadi pale watakapokamilisha ujenzi wa machinjio ya kisasa.

Rais Magufuli amesema hayo, alipofanya ziara ya kushtukiza na kuwataka viongozi wa Halmashauri hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na watendaji wengine kuangalia namna ya kukamilisha kazi hiyo ili kuwaondolea adha wafanyabiashara wa maeneo hayo.

Amesema, kuanzia sasa mkurugenzi wa Halmashauri na watendaji wengine ni marufuku kukusanya mapato ya aina yoyote sambamba na kuwataka kufanyia kazi maagizo yake usiku na mchana.

Uamuzi huo umepokelewa kwa shangwe na wafanyabiashara wa eneo hilo la machinjioni ambalo linadaiwa kukusanya takribani milioni 100 kwa mwezi baada ya kupita akitokea kwenye uzinduzi wa Rada na kiwanda cha mabomba ya plastiki kilichopo maeneo ya Vingunguti jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...