Search This Blog
Tuesday, July 23, 2019
Harmonize Afunguka Tetesi za Kuwa Amemsign Q Chief Kwenye Lebo yake
Msanii kutoka WCB Harmonize anayetamba na wimbo wake wa My Boo aliomshirikisha mkongwe wa muziki wa bongo fleva Q Chief amesema kuwa ‘hajamsaini’ msanii huyo bali amemsaidia gari aina ya Porte kwaajili ya usafiri ambao utamsaidia katika kazi zake za muziki.
Harmonize ambaye ametoa mfululizo wa nyimbo zake yaani EP siku ya jana akiwa amemshirikisha Q Chief, amesema kuwa tatizo la Q Chief ni la kijamii hivyo hatakiwi kuachwa peke yake kwani ni msanii ambaye alikuwa anaushawishi kwa vijana wengi kuingia katika muziki na kuna ambao tayari wamepata matunda ya sanaa ya muziki.
Aidha, amesema kuwa, mkongwe huyo wa muziki wa bongo fleva atakuwepo katika tamasha la wasafi festival ambapo watatumbuiza nyimbo alizomshirikisha katika mfululizo wa nyimbo ‘EP’ katika jukwaa la wasafi festival.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment