Search This Blog

Sunday, June 2, 2019

Watu 10 Wameuawa Katika Shambulio la Kujitoa Muhanga

Kwa mujibu wa Shirika linaloangalia #HakiZaBinadamu nchini Syria mlipuko huo ulisababisha vifo vya raia watano na Wanajeshi watano wa kundi la Syrian Democratic Forces(SDF)

Watu wengine 20 wamejeruhiwa katika mlipuko huo wa kujitoa muhanga uliotokea Jumamosi mjini Raqa, ngome ya zamani ya Wanamgambo wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, Kaskazini mwa Syria

SDF ni kundi la muungano wa Wakurdi na Waarabu linaloungwa mkono na Marekani, na ambalo lilipambana kuukomboa mji huo kutoka kwa IS mnamo Oktoba 2017

Shambulio hilo ambalo hakuna kundi lililodai kuhusika, lilitanguliwa na mlipuko wa bomu uliosababisha watu kadhaa kujeruhiwa katika eneo jingine la mji huo ambalo mara kwa mara hushambuliwa na Wanamgambo wa kundi la Dola la Kiislamu  



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...