Search This Blog
Sunday, June 2, 2019
Trump ataka Uingereza ijiondoe katika Umoja wa Ulaya
Rais wa Marekani Donald Trump amesema Uingereza inapaswa kukataa kulipa pauni milioni 39 kama malipo ya kujiondoa katika Umoja wa Ulaya, na pia ameishauri ijiondoe katika mazungumzo ya Brexit iwapo umoja huo utakataa kuipa nchi hiyo inachokitaka.
Katika mahojiano na gazeti la Sunday Times kabla ya ziara yake rasmi nchini Uingereza itakayoanza Jumatatu, Trump amesema Waziri Mkuu ajaye amtume Nigel Farage - anaeunga mkono nchi hiyo kujiondoa katika Umoja wa Ulaya - kuiwakilisha Uingereza katika mazungumzo ya Brexit mjini Brussels, Ubelgiji. Trump amesema Uingereza inapaswa kujitoa katika Umoja wa Ulaya mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment