Search This Blog
Monday, June 3, 2019
Mwanaume Ajiua Baada ya Kunyimwa Pesa ya Pombe na Mkewe
James Kamau (39) mkazi wa kijiji cha Mbogo-ini kaunti ya Murang'a amejiua baada ya kunyimwa pesa ya kwenda kunywa pombe na mke wake.
Kamanda wa Polisi wa Murang’a, Josephat Kinyua amesema mwanaume huyo baada ya kutoka kwenye shughuli alizokuwa akizifanya, alipitia bar na rafiki yake na kuanza kunywa pombe huku yeye akiwa mlipaji, lakini alipomaliza pesa alirudi nyumbani na kutaka mkewe ampatie pesa nyingine.
Alizua fujo akitaka apewe pesa kwa lazima, baada ya mama yake kusikia vurugu hizo, alimchukua mke wa Kamau na kumpa malazi.
Kwa hasira, Kamau alisikika akimuonya mama yake kuwa alikuwa na upendeleo kwa mkewe na akaapa kuwaadhibu wote wawili kwa maombolezi kisha akafunga mlango na asubuhi yake watoto walimkuta baba yao akining’inia kwenye paa la nyumba sebuleni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...

No comments:
Post a Comment