Search This Blog

Wednesday, May 29, 2019

RC CHALAMILA ALITAKA BARAZA LA BIASHARA KUWA KIUNGO MUHIMU KATI YA SERIKALI NA SEKTA BINAFSI.

Na Emanuel Madafa,Mbeya 

Serikali imeliataka baraza la biashara Mkoa wa Mbeya kuanza majadiliano ya pamoja kati ya sekta binafsi na serikali kuhusu masuala ya uwekezaji.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila wakati akizingumza na wajumbe baraza jipya la biashara Mkoani Mbeya .

Amesema lazima kuwepo na majadiliano ambayo yatawezesha wawekezaji wa ndani na nje ili kufahamu sera na vikwazo Mbalimbali katika hatua za uwekezaji.

“Kati ya sekta binafsi na sekta za umma inapotokea tunafanya kazi kwa pamoja kwa njia ya majadiliano kunauwezekano mkubwa tukajadili changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa kikwazo kwa wawekezaji hasa masuala ya tozo na kodi “Amesema Chalamila 

Ameeleza kuwa sekta binafsi inaweza kuwa na mchango kubwa kwa kuishauri serikali juu ya mazingira bora ya uwekezaji.“Serikali ikiwa imenyamaza na kutumia mabavu katika kuendesha manaake itabidi sasa watu wasiwe wawekezaji wala wafanyabiashara “Amesema Mkuu wa Mkoa .

Aidha Chalamila amelitaka baraza hilo kuandaa na kutoa taarifa kwa wawekezaji kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika Mkoa wa mbeya .

Kwa wake Mwenyekiti wa Chama Cha wenye viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mbeya Dkt . Lwitiko Mwakalukwa amesema baraza la biashara ni muhimu zaidi kuwepo hasa katika Maendeleo ya biashara na uwekezaji Nchini.
 Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (Mwenye shati jeupe) katika picha ya pamoja na wajumbe wapya wa baraza la biashara Mkoa Mbeya
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh Albert Chalamila akizungumza na wajumbe wa Baraza jipya la biashara Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani)katika Ukumbi wa Mkapa .

 Wajumbe wapya wa Baraza la wafanyabiashara Mkoa wa Mbeya .
 Mwenyekiti wa Chama Cha wenye viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Mkoa wa Mbeya Dkt . Lwitiko Mwakalukwa akizungumza na wajumbe wa  baraza jipya  la biashara ambalo limeanza kazi mara baada kupatikana kwa wajumbe wapya.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...